Participation of Samia Suluhu Hassan to the One Ocean Summit in Brest on 11 February 2022 - Rais Samia Suluhu Hassan ashiriki Mkutano wa Bahari Moja jijini Brest februari 11, 2022 [fr]

JPEG

English:
« Ocean is a common good ». President Samia Suluhu Hassan spoke at the high-level segment of the One Ocean Summit which brought together more than forty heads of state or government in Brest on 11 February 2022. “By advancing ocean governance, nations will be able to deal with issues, which pose a threat to the ocean like illegal fishing, climate change, overexploitation and marine pollution”, she pointed out. The leaders came away with an oft-repeated message: action must be accelerated to contain or avoid as much as possible the damage of climate change, especially on biodiversity. Watch her full speech in the video below. Its transcript is also available.

Zip - 33.2 Mb
(Zip - 33.2 Mb)

Thank you for this chance and I appreciate being here attending the conference on how we are going to govern our oceans.

I have been hearing the word "governance", but then I have been hearing "good governance", and, the good governance on our country’s politics, and good governance on our resources, but it is very rare to hear ocean governance.

I am just starting to hear about ocean governance, for me when we talk about ocean governance, it brings a lot of ideas on my head; because when we talk about ocean governance, this means the ocean is a transboundary property, which is owned by different countries in the world, it is a common property, and by the governance that means we have to have a very strong mechanism of coordination, the way we are going to share it , the way we are going to use ocean resources, and, how can we mutually benefit from the resources in there, and, how can we protect this property together. So I think for the developing countries there is a lot to learn about ocean governance.

I have listened to the previous speakers when they talk about scientific findings of the oceans, and we say we know all these findings, and, we have to take actions. But on the other part of the world these findings are not there, we do not know these findings, I think first of all we need to share the knowledge about the scientific finds of the ocean and how can we all be aware of what has to be done so as to have the good governance of our oceans, and I think I am here to learn from others about I have to start by saying this, and thereafter I might be coming back again when I hear other people’s contributions but for us the LDCs in Tanzania specifically, we are ready to protect the ocean but there gain there is a lot to be shared with us and probably with other countries.

Thank you for this chance, thank you very much.

Swahili:
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, alihudhuria kilele cha mkutano wa unaohusu rasilimali bahari (One ocean Summit) uliofanyika Februari 11, 2022 mjini Brest Ufaransa uliowakutanisha viongozi mbalimbali wa Nchi zenye ukanda wa rasilimali bahari kufuatia mualiko wa Rais wa Jamhuri ya Ufaransa Emmanuel Macron.
Katika hotuba yake Rais Samia amemshukuru Rais Macron kwa fursa ya kushiriki mkutano huo utakaoonesha namna ya kuzitawala na kuzilinda bahari kwa manufaa.
Rais Samia amesema amekuwa akisikia neno "utawala", "utawala bora", utawala bora juu ya siasa za nchi yetu, utawala bora kwenye rasilimali zetu, lakini ni nadra sana kusikia utawala wa bahari.
"Naanza kusikia kuhusu utawala wa bahari, kwangu tunapozungumzia utawala wa bahari, huleta mawazo mengi kichwani, kwa sababu tunapoongelea utawala wa bahari hii ina maana bahari ni rasilimali inayovuka mipaka ambayo inamilikiwa na nchi mbalimbali duniani ni mali ya pamoja na kwa mantiki hiyo maana yake ni lazima tuwe na utaratibu madhubuti sana wa uratibu wa shughuli za baharini" amesema Rais Samia.
Rais Samia amebainisha mbinu atakazotumia jinsi ya kushiriki na namna atakavyowezesha kutumia rasilimali za bahari vyema.
"Tunawezaje kufaidika kutokana na rasilimali zilizomo baharini, na tunawezaje kulinda mali hii pamoja.
Kwa hiyo nadhani kwa nchi zinazoendelea kuna mengi ya kujifunza kuhusu utawala wa bahari nimewasikiliza wazungumzaji waliotangulia wanapozungumza kuhusu matokeo ya kisayansi ya bahari, na tunasema tunajua matokeo haya yote, na tunapaswa kuchukua hatua" amesema Rais Samia.
Rais Samia amekiri kwamba, kwa upande mwingine wa ulimwengu matokeo haya hayapo, na hatuyajui, na kusema kuwa anadhani kwanza kuna haja ya kupeana maarifa juu ya ugunduzi wa kisayansi wa bahari na ufahamu wa kipi kifanyike ili kuwe na utawala bora wa bahari zetu.
Aidha Rais Samia ameahidi kushirikiana vyema na mataifa mengine juu ya matumizi bora ya rasilimali bahari "Nipo hapa kujifunza kutoka kwa wengine sina budi kuanza kwa kusema hivyo baada ya hapo naweza kurudi tena kusikiliza michango ya watu wengine lakini kwetu sisi LDCs nchini Tanzania, tupo tayari kulinda bahari kwani kuna faida kubwa na mengi ya kushiriki nasi na pengine na nchi zingine" amesema Rais Samia.
Ameshukuru kwa fursa hiyo, ameshukuru mno.

Dernière modification : 14/02/2022

top of the page